MRAJIS WA VYAMA VYA USHIRIKA NCHINI DKT. BENSON NDIEGE ATEMBELEA BANDA LA MAONESHO YA NANE NANE LA SHIRECU - JIJINI DODOMA

Mrajis wa Vyama vya Ushirika nchini, Dkt. Benson Ndiege akipokea zawadi kutoka kwa Meneja Mkuu wa SHIRECU, Bw. Alpha Makasi, alipotembelea banda la SHIRECU (1984) LTD katika Maonesho ya Nane Nane 2026, jijini Dodoma. Aidha Mrajis amefurahishwa na namna Shirecu inavyojiendesha kwa sasa, uwekezaji unaoendelea kufanyika, miradi ya maendeleo inayofanyika hususani Duka la pembejeo, Viwanda vya Kuchakata Pamba Pamoja na uendelezaji wa Shule ya Sekondari ya Buluba

Katika Maonesho ya Nane Nane mwaka huu, Shirecu Ltd imekuja na Fursa mbalimbali za uwekezaji katika Viwanda, biashara, kilimo cha Pamba, Kilimo cha Choroko, Kilimo cha Dengu zinazolenga kuimarisha sekta za kilimo na Ushirika kwa Ujumla. Fursa hizi zinawalenga Watanzania wote na watu kutoka mataifa mbalimbali wanaotamani kuwekeza na SHIRECU.

Tunakukaribisha kutembelea banda letu la Shirecu Ltd lililopo katika Kijiji cha Ushirika, Maonesho ya Nane Nane 2026 Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma, ujionee bidhaa, fursa za uwekezaji na uzalishaji unavyofanyika SHIRECU.

Go Back